Sunday, October 28, 2007

Mradi wa mabasi yaendayo kasi ni kitendawili kigumu


TATIZO LA USAFIRI DAR BADO NI KITENDAWILI
18th January 2007, 01:27

Kwa wakazi wa Dar na vitongoji vyake taarifa hii ni kukatisha tamaa, kutokana na usumbufu wanaoupata kila asubuhi na jioni kugombania daladala nathubutu kusema hatuna serikali na kama ipo imekwenda likizo.


Mobini Sarya

KAMA kuna kitu ambacho wakazi wa Dar es Salaam, walikuwa wanakisubiri kwa hamu na kwa muda mrefu, ni mradi wa usafiri mpya wa mabasi yaendayo kasi, uliotarajia kuanza mapema mwaka huu.


Usafiri jijini Dar es Salaam, ambako asilimia saba ya Watanzania wanaishi wakisaka maisha, unatajwa kuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi.Kutokana na kukosekana usafiri wa uhakika katika jiji hili, inakisiwa kuwa, wakazi wake hupoteza wastani wa saa zaidi ya tatu kwa siku nje ya ofisi zao.

Pia inakisiwa kuwa, asilimia 70 ya pato la taifa, huzalishwa kwenye jiji hili,lakini pamoja na umuhimu huo, mapato yanayopatikana yameshindwa kutumiwa vyema kuboresha miundombinu ikiwamo barabara ambazo nyingi ni zile zilizojengwa wakati wa uhuru.Tatizo la usafiri Dar es Salaam, kushindwa kutatuliwa na mamlaka zinazohusika, ni kielelezo tosha cha uwajibikaji hafifu kwa baadhi ya watendaji, hasa katika maeneo fulani yaliyobinafsishwa.


Kwa mfano tangu serikali ilipojitoa kwenye sekta ya usafiri jijini Dar es Salaam na kuamua kuikabidhi Kampuni ya Usafiri jijini humo (UDA) kwenye sekta binafsi,kampuni hiyo imeshindwa kuleta matumaini.Hadi sasa, inakisiwa kuwa wastani wa abiria 123,000 hutumia usafiri wa daladala, ambazo zinakadiriwa kufikia 9,300, zinazotoa huduma kwa siku, huku ikikadariwa kuwa, abiria zaidi ya 100,000 hukosa usafiri huo.

Aidha, husafirikwa miguu, baiskeli, pikipiki, gari ndogo na hata kupanda malori ya mizigo. Katika uchunguzi uliofanywa mwaka 2004, ilibainika kuwa kila siku daladala moja hupoteza sh 6,000 sawa na sh 180,000 kwa mwezi, ambazo hutumika kuwalipa wapiga debe.

Pesa hizo kama zingekusanywa na Chama cha Wamiliki wa Daladala (TABOA), kwa daladala 9,300, wangepata zaidi ya sh milioni 55 kwa mwaka.Pesa hizo zingeunda kampuni ya usafirishaji jijini (KAUJI) na wengeweza kuzitumia kama dhamana kupata mkopo ili kuagiza mabasi mengi makubwa.


Kutokana na umuhimu huu wa usafiri wa jiji, serikali imekuwa ikilaumiwa kwa kushindwa kuuoboresha kwa kupanua miundombinu ili watu wawe wanawahi kazini na wanafunzi wanawahi mashuleni ili taifa lipate maendeleo.
Ndio maana Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam, ikaamua kubuni na kutangaza kuanzisha mradi wa usafiri wa mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (Dar Rapid Trans - DART), ambao kila mara wamekuwa wakiwatangazia wananchi kuwa ungeanza mapema mwaka huu.

Wananchi wanashangaa na wanashindwa kupata majibu kamili, ilikuwaje taarifa zilikuwa zikitolewa na kuwapa watu matumaini, wakati mradi huo ambao unasubiriwa na wengi haujawa tayari? Taarifa hizo zilianza Agosti mwaka jana, kwamba mradi huo wa DART ungeanza kutoa huduma, lakini haikuwa hivyo.

Mradi huo, unasimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, mwishoni mwa waka jana ilitolewa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa, mradi huo ungeweza kuanza kazi Machi, mwaka huu.
Wananchi wakazidi kuvuta subira, hasa wale wa Mabagala na Gongo la Mboto, ambao usafiri mzuri kwao ni anasa na kupita kwenye madirisha ya mabasi wala si jambo la kushangaza.Taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa, inaonekana kuwa usafiri huo utakuwa wa usalama, uhakika na wa haraka hali inayowapa matumaini makubwa wakazi wa Dar es Salaam.


Wakati tulipokuwa tukiambiwa mradi unaanza mwezi wa Agosti, mara mwaka kesho, ulikuwa ni wimbo mtamu ambao msikilizaji alikuwa hauelewi vema.
Aidha, mwimbaji alikuwa anatumia ujanja kumliwaza msikilizaji hata kama wimbo huo ulikuwa unaimbwa kwa mafumbo.
Wanasema kuwa, unaweza kuwadanganya watu wote, lakini si kwa wakati wote, huo msemo ndio ulinifanya nikapiga hodi kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam ili nifahamu ukweli wa mradi huu kwamba utaanza lini.Nilipofika kwenye ofisi hiyo, haikuwa kazi rahisi kupata taarifa, kwani ofisa niliyekutana naye kwenye ofisi za kitengo hicho, hakuwa tayari kutoa ukweli huo na hata habari hizo hazikumfurahisha, baada ya kufahamu kuwa nilikuwa nataka kujua ni lini usafiri huo utaanza rasmi.Baada ya mabishano ya muda mrefu, hatimaye tulifikia mwafaka na akanipeleka kwa ofisa mwingine aliyeniahidi kuwa, nirudi baada ya mwaka mpya ili aweze kunipatia taarifa kamili, sikufanya ubishi, niliondoka na mwaka mpya ulipoanza nilikwenda tena kwenye ofisi hizo.

Wakati najaribu kufuatilia habari hii, kichwani nilikuwa najiuliza habari ya mradi mwingine wa kuzalisha umeme, uliokabidhiwa kampuni moja ya nje yenye jina la Richmond, ambao wasemaji wake walikuwa wakipiga danadana tarehe ya uhakika ya kuanza kuzalisha umeme.

Baada ya kufika, nilikabidhiwa ripoti kamili iliyoandaliwa Desemba 5, mwaka jana kutokana na kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Temeke na kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam, wadau pamoja na mkuu wa mkoa.

Kwenye mkutano huo, ambao walialikwa pia waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro, akitoa hotuba yake alisema miundombinu kwa ajili ya mradi huo inatarajiwa kuanza mwaka huu, na huduma ya usafiri itaanza kutolewa rasmi mwaka 2009, kisha akamaliza kwa kusema
“hatutarajii mipango isiyo na mwisho, tunataka matokeo.”

Lakini pamoja na taarifa hiyo kubainishwa kwamba usafiri utaanza rasmi mwaka 2009, taarifa ambazo zilitoka kwenye vyombo vya habari, zilikuwa zinabainisha kuwa, huduma hii ya usafiri wa mabasi yaendayo kwa kasi itaanza Machi mwaka huu.

Taarifa kwenye vyombo hivyo zilisisitiza pia kuwa, hata daladala ndogo zitapigwa marufuku kuingia katikati ya jiji, baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wameagiza magari hayo, waliingiwa na hofu na hata wengine wakarudisha magari waliyokuwa wameagiza kwa hofu kuwa huenda yangeshindwa kufanya kazi.Hakuna lililoendelea, mambo hayo ni sawa na tunda bichi ambalo halijawa tayari kuliwa.


Ukweli ni kwamba, kama kuna wafanyabiashara waliokuwa wamesita kuagiza magari ya kutolea huduma, ni bora wakabadilisha msimamo wao na kuagiza magari hayo, kwani ukweli ni kuwa, mradi huo unaelezwa kuwa, unatarajiwa kuanza kutoa huduma kuanzia Machi 30 mwaka 2009 kwa kutumia mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria 140 na 160, tena kwa kuanzia katika Barabara ya Morogoro tu.

Mpango mzima wa mradi huo na ambao labda unaweza kumaliza tatizo la usafiri jijini, unatarajiwa kukamilika mwaka 2035, kutokana na mpango huo kugawanywa katika awamu sita, ambazo zina jumla ya kilometa 137, ambazo barabara na miundombinu mingine itakuwa ikitengezwa kwa awamu.

Kutokana na ripoti hiyo, inaonekana kuwa, kuanzia Machi 2007 wataalamu wa mradi huo wataanza kusanifu barabara zenye kilometa 20.9 ambazo zitahusisha vituo vya Kimara, Ubungo, Morocco, Kariakoo na Kivukoni katika zoezi hilo litakalokwenda sambamba na kufanyia tathmini
wale wote wanaopaswa kulipwa fidia ya kuhamishwa ili kupisha ujenzi wa barabara mpya,

ambazo zitatumiwa na mabasi hayo.Shughuli hii inatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu
na ujenzi wa awamu ya kwanza ya mradi unatarajiwa kugharimu sh bilioni 122, ambazo zinatolewa na Benki ya Dunia na watakaoshughulika na ujenzi huo ni Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).

Awamu hiyo ya kwanza ya mradi itakuwa na barabara yenye urefu wa km. 20.9 na itakuwa imegawanyika katika sehemu kuu tano, ambazo ni zile za wanaokwenda kwa miguu, baiskeli, magari ya watu binafsi vituo vya daladala nyingine na vile vya mabasi hayo maalumu. Nauli

ambazo zinapendekezwa mradi huu ukikamilika ni kati ya sh 200 na 300 hadi 500 mpaka mwisho wa safari.Tathimini iliyofanywa mwaka 2004, ilibainika kuwa, Barabara ya Morogoro inaongoza kwa kupitiwa na magari mengi na ndipo mradi utakapoanzia na baada ya hapo

itafuatia Barabara ya Kilwa ambayo nayo inatumiwa zaidi.Mradi wa awamu ya pili utakaohusisha barabara hiyo utaanza mwaka 2012 ukiwa na kilometa 19.3 na awamu ya tatu itakuwa mwaka 2016 ukiwa na barabara ya km. 23.6.Awamu ya sita na ya mwisho inatarajiwa

kukamilika mwaka 2035 takribani miaka 10 baadaye, kama mipango itakwenda kama inavyoelezewa na kama yatazingatiwa maneno ya Kandoro aliyosema kwa ‘hatutarajii kuwa na mipango isiyo na mwisho’, lakini vilevile itategemea sera ya viongozi wanaofuata miaka kumi inayokuja.

Kwa hali yoyote ile, kukamilika kwa mradi huu ni sawa na mwenye njaa anayesubiri matunda yaive ndipo ale, kama mradi huu unategemea fedha za wafadhili ndio utekelezwe, matumaini yake ni madogo, na hata kama ni wawekezaji, basi wasiwe na sura ya Richmond, ambao

wataendeleza yale ya ngoja leo ngoja kesho.Kulingana na maelezo ya mradi huu unaotarajiwa kukamilika mwaka 2035, amabako wengi hatutarajiwi kuwapo hai, tungeomba serikali itazame njia haraka na mbadala kama ya usafiri wa baharini na kuingia ubia na mwekezaji mpya wa TRC
ili aweke usafiri wa reli kupita maeneo ya jiji ili kuondoa adha kwa wananchi.

haya ni baadhi ya maoni ya wasomaji waliochangia;PADINGTON GREEN2nd February 2007, 03:08 AM

Ndg yangu usijidanye kwa mradi huo, hapo pana mkono wa mtu ambaye alitaka kuondoka vipanya hapo Tanzania hasa Dar, lakini amekumbana na wakati mgumu kwani hata hao vigogo wengi wao wana vipanya hivyo, pia hautakuwa Dar rapid trans (DRT) badala yake hata ukianza

utaitwa jina jipya yaani Dar slow moving Trans, kwani ili hayo magari yaende kasi lazima pawepo na barabara special kwa hayo mabasi kwa maeneo ya central district area yaani bus lane je itawezekana utapanuaje hizo njia za nyoka hapo Dar?ni kitu kama ndoto.... au ni sawa na

unavyo nunua tiketi ya LOTTO kwa mategemeo ya kupata mamilion probability yake ni ndogo sana 0.000000000001. angalia hapo nini kingine kifanyike badala ya kufikiria Dar rapid trans


Morani7519th July 2007, 08:55 AM

Heshima kwa wote....Naona wenzangu wameliangalia suala hili la "Dar Rapid Trans" na kwa kweli sishangai kuona kuwa kuna wenzangu ambao

ingawa mradi huu umeshaanza utekelezwaji, bado kuna watu bado tuna wasiwasi na ufanisi wake mara utakapokamilika. Tatizo ni kwamaba kumekuwa na tabia ya usiri sana kwenye serikali yetu.

Usiri ni mzuri kama ni kuhusu masuala ambayo yana manufaa kwa watu wengi lakini sio lazima liwe linajulikana kwa watu wengi, "issues of national inteligence".Sasa mfano rahisi ni lile suala la DRT, 3 by 1 use of major arterials (double roads) wakati wa peak hours.

Kwa kweli pamoja na kwamba miradi hii inahusishwa watu wengi, ikiwemo watembea kwa miguu, waendeshaji wa magari, wenye kutumia baiskeli/pikipiki/tairi tatu na usafiri mwingine; wengi wao hawakushirikishwa kwenye maamuzi ndio maana wengi tulisikia kuhusu mambo ya watu kugongwa na magari, ajali za magari kwa magari nk.

Sasa kamavyombo vya serikali vinaimgia kwenye miradi mikubwa inayogusa kada zote za jamii ni bora na lazima wawekezaji na watumiaji wote washirikishwa hata kama ni kupata views ambazo hazitakuwa na uzito sana and decide on the final implementation plan based on weighted

average of views and not based on some few individuals and what we call consultants who came from outseide the country on sorting out traffic problem for people coming from Mbagala.

Kama unataka kutatua tatizo la usafiri Mbagala, usitegemee mtu wa Kigogo au Tandika kutatua tatizo hilo. It is a high time that we try and use peoples views no matter small and so called ilogical in solving their views.

We have all learnt from EAC fast tracking, though wengin walisema itakuwa ni a fluke na tutalazimishwa kuingia kichwa kichwa, wote tumeona mafanikio ya watu wengi (>70%) saying, NO WE ARE NOT READY NOW.........Watanzania tuamke na kujenga nchi yetu, Haba na Haba Hujaza Kibaba.....Koba

19th July 2007, 12:22 PM Morani

its OK unachosema lakini naona unaingiza politics kwenye vitu vinavyohitaji expert's/pro's...urban transportation system ni very complex kuliko unavyofikiria,wenzetu walioendelea wanatumia computer models to solve hili tatizo na ni software ambayo inacost pesa nyingi..

kwa population ya 3m plus ujue vikao vya wananchi au politicians hawataweza kusolve hilo tatizo,its time now to use really experts and stop all the BS...issue ya Dar imefikia pagumu sana na wasipofanya kazi yao NATURE itafanya kazi yake...WAIT & SEE what i mean by sayingNATURE!Morani75

19th July 2007, 02:11 PM Koba,
nashukuru kwa ushauri wako mzuri kuhusu mada hii. Lakini, unavyosema naingiza siasa, inakuwa ni ngumu kidogo.

Inaelekea niliposema tutumie washika dau (stakeholders) sio siasa ndugu yangu....Hata kwenye nchi zilizoendelea kama ulivyosema kuwa wanatumia simulation (softwares) usifikiri kuwa computer software inaamua bila kuwa na inputs.Among he inputs ni hizo hoja za washika dau

ambazo zinakusanywa mara nyingi through "questionnaires" na zinakuwa part of the input parameters.

Kwa hiyo ndugu yangu sio siasa, na wala computer traffic simulation softawares (many are available i.e. ITS, PTISP) haziwezi fanyakazi bila parameter inayokuwa derived from people/users comments (which includes pedestrians, drivers, commuters, cyclists and to be

sincere even in some areas farmers (cattle keepers as for the case of high speed highways/cross countries through vast farm lands which at times are provided with animal crossings underpasses)!!Ndugu yangu, information technology (design and other softwares) ni kama

chungu, kitakachoiva kinategemeana na zile constituents/viungo na vingenie ulivyoweka mwanzo wa mapishi.Huwezi weka mchele na kunde utegemee kupata pizza sababu nchi zilizoendelea wanapata pizza, wao wametengeneza chungu chao kuweza kutambua parameters kwa ufanisi lukuki kuweza kusaga na eventually kuwatolea pizza.

Sasa chungu chao kinaweza work kwao lakini kwetu inategemea na aina ya kunde, mchele etc ambazo zinatokana na ideas za walaji(stakeholders for that case) through questionnaires!!!Naomba kuwakilisha....katibu tarafa19th July 2007, 05:03 PM75,tatizo la usafiri dar ni la muda mrefu,viongozi wanafikiri bado wapo kwenye kampeni.

kwamaoini yangu,chukua barabara ya morogoro/mandela pale inatakiwa wajenge tannel kwa wale wanao toka kimara kwenda mjini wapite juu au chini na nafasi ya kufanya hivyo bado ipo,alikadhalika pale


kilwa/mandela,changombe/mandela,hata tazara pale nyerere/mandela.na kuna sehemu zingine nyingi tu wanaweza kufanya hivyo na tukapunguza foleni.DAR si LAMU19th July 2007, 10:25 PMHeshima kwa wote....Naona wenzangu wameliangalia suala hili la "Dar Rapid Trans" na kwa

kweli sishangai kuona kuwa kuna wenzangu ambao ingawa mradi huu umeshaanza utekelezwaji, bado kuna watu bado tuna wasiwasi na ufanisi wake mara utakapokamilika. Tatizo ni kwamaba kumekuwa na tabia ya usiri sana kwenye serikali yetu.

Usiri ni mzuri kama ni kuhusu masualaambayo yana manufaa kwa watu wengi lakini sio lazima liwe linajulikana kwa watu wengi,"issues of national inteligence". Sasa mfano rahisi ni lile suala la DRT, 3 by 1 use of major arterials (double roads) wakati wa peak hours.


Kwa kweli pamoja na kwamba miradi hii inahusishwa watu wengi, ikiwemo watembea kwa miguu, waendeshaji wa magari, wenyekutumia baiskeli/pikipiki/tairi tatu na usafiri mwingine; wengi wao hawakushirikishwa kwenye maamuzi ndio maana wengi tulisikia kuhusu mambo ya watu kugongwa na magari, ajali zamagari kwa magari nk.

Sasa kama vyombo vya serikali vinaimgia kwenye miradi mikubwa inayogusa kada zote za jamii ni bora na lazima wawekezaji na watumiaji wote washirikishwa hata kama ni kupata views ambazo hazitakuwa na uzito sana and decide on the final implementation plan based on weighted average of views and not based on some few individuals and what wecall consultants who came from outseide the country on sorting out traffic problem for people coming from Mbagala.


Kama unataka kutatua tatizo la usafiri Mbagala, usitegemee mtu wa Kigogo au Tandika kutatua tatizo hilo. It is a high time that we try and use peoples views no matter small and so called ilogical in solving their views.We have all learnt from EAC fast tracking, though wengin walisema itakuwa ni a fluke na tutalazimishwa kuingia kichwa kichwa, wote tumeona mafanikio ya watu wengi (>70%) saying, NO WE ARE NOT READY

NOW.........Watanzania tuamke na kujenga nchi yetu, Haba na Haba Hujaza Kibaba.......kama kawaida naona wananchi wanatajwa!yapatikane maoni toka kwao!..nadhani hii si politics mhe.,

hapa wataalamu wanahitajika kufanya kazi yao ambayo itabidi iheshimiwe,hasa na ninyi waheshimiwa...huu mradi umeanza kutekelezwa kwenye vikao,majukwaa ya kisiasa,kwenye semina,na makaratasini,lakini on the ground bado...sasa,si wengine ni wakina thomaso,hatuweziamini yesu aliyesulubiwa kafufuka mpaka tutie kidole sehemu alochomwa mkuki!..



ngoja tutatia kidole kuona barabara ya kilwa itakapokamilika!haya ni maoni ya wasomaji waliochangia makala hii ambayo ilitoka kwa mara ya kwanza katika gazeti la Tanzania Daima kabla ya kutumika kwenye mtandao wa Jambo forum ambapo wadau w alipata nafasi ya kuchangia maoni yao kuhusu huu mradi.


Posted by apex chamber at 7:46 AM 0 comments
Labels:
Subscribe to: Posts (Atom)
Blog Archive
2007 (2)
October (2)
AGIZO LA KUACHA KUPAKIA ABIRIA ZAIDI LAPUUZWA
TATIZO LA USAFIRI DAR BADO NI KITENDAWILI

About Me
apex chamber View my complete profile

AGIZO LA KUPAKIA ABIRIA ZAIDI LAPUUZWA


AGIZO LA KUACHA KUPAKIA ABIRIA ZAIDI LAPUUZWA


Agizo la kuacha kupakia abiria zaidi katika mabasi lapuuzwa 2007-07-18 20:09:17 Na ITV HabariAgizo la waziri mkuu la kutaka mabasi ya abiria kutozidisha abiria ili kuepusha ajali bado linapuuzwa na baadhi ya wasafirishaji wilayani Kondoa. Baadhi ya mabasi ya kampuni moja ya usafirishaji yameonekana kuwa ndiyo yanayoendekeza tabia hiyo kwa kile baadhi ya abiria walichoeleza kuwa ni kuogopwa na askari wa usalama barabarani. ITV imeshuhudia mkuu wa wilaya hiyo kepteni Seif Mpembenwe akizuia basi moja lililokuwa limesheheni abira hadi katika sehemu ya mizigo, huku wengine wakining`inia.SOURCE: ITV